Nenda kwa yaliyomo

Mchezo wa video

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtoto akicheza kwa kutumia kiweko video.

Michezo ya video ni michezo elektroniki inayochezwa kwenye skrini inayoweza kupatikana kwenye runinga, kompyuta au kifaa kingine.

Kuna aina nyingi za michezo hii: michezo ya kuiga majukumu mbalimbali, ya kupiga bunduki, ya kuendesha mbio magari na mengine mengi.

Michezo ya video kwa kawaida hupatikana kwa njia ya diski au upakuaji wa dijiti. Kifaa maalum kinachotumiwa kucheza mchezo wa video nyumbani huitwa kiweko video. Kulikuwa na aina nyingi za viweko video na kompyuta zilizotumika kucheza michezo ya video. Kati ya zile za kwanza zilikuwa Atari 2600, Sega Master na Nintendo kwenye miaka ya 1980. Kiweko video kulichouzwa zaidi duniano ni PlayStation 2 iliyotengenezwa na Sony.

Mchezo wa video Arcade.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mchezo wa video kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
OSZAR »